Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe ametoa wito kwa wananchi wa kata ya Imalinyi kuweza kushiriki kuchangia nguvu katika ujenzi wa Kituo cha Afya kinachojengwa katika kata hiyo,Mhe Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo leo Tarehe 17/3/2022 akiwa katika kata ya Imalinyi akizindua ujenzi wa Kituo cha afya. “Ninawaomba sana Wananchi muweze kujitolea kwa kiasi kikubwa nguvu zenu ili ujenzi wa kituo hiki cha afya unaojengwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu uweze kukamilika kwa haraka ili kuunga jitihada za Serikali “ Alisema Mhe Mkuu wa Wilaya Lautery John Kanoni.
Hafla ya uzinduzi ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mhe Agnetha Mpangile Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe Diwani wa Kata Mhe Onesmo Lyandala,Mganga Mkuu Dr Frank Chiduo, na Mtendaji wa Kata hiyo Jovitha Sanga
Mhe Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe amesema Serikali katika jitihada zake za kuboresha huduma za afya imeleta Fedha Tsh 250,000,000/= kwa ajili ya ujenzi wa Kituo hicho na Serikali itaendelea kuleta fedha nyingine ili kukamilisha kiasi cha Tsh 500,000,000/= ambazo ndio kiasi cha fedha kinachoweza kukamilisha majengo saba yanayotakiwa kujengwa.
Nae Mheshimiwa Diwani wa kata ya Imalinyi Mhe Onesmo Lyandala ametoa Shukrani zake kwa Serikali ,Mbunge Mhe Festo Dugange kwa kuhakikisha Kituo cha Afya iImalinyi kinajengwa amemhakikishia Mhe Mkuu wa Wilaya kuwa wananchi wa Imalinyi wapo tayari na wameupokea Mradi kwa moyo mweupe na wapo tayari kuchangia nguvu zao ili kuona Mradi unakamilika na ikiwezekana kufanya na jambo jingine katika ujenzi huo.
Aidha akielezea utaratibu wa Ujenzi huo Mganga Mkuu wa Wilaya Daktari Frank Chiduo amesema majengo yatakayo jengwa ni majengo saba yenye thamani ya Tsh 500,000,000/= ikiwa ni Jengo la wagonjwa wa nje,Jengo la Mama na Mtoto, Jengo la Upasuaji,Jengo la Maabara,Jengo la kuhifadhia Maiti, Jengo la Kufulia na Nyumba ya Mtumishi kwa sasa utekelezaji unaanza na Ujenzi wa Jengo la Wagojwa wa nje yaani OPD.
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.