Vijana 246 wa maeneo mmbalimbali ya Wilaya ya Wanging’ombe wameaswa kuwa wazalendo katika kutekeleza zoezi la Anwani za Makazi, hayo yamesemwa na Mhe Mkuu wa Wilaya yaWanging’ombe wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya uandishi wa namba kwenye nyumba na kuchukua Taarifa za anwani za makazi yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe.”Kazi hii ni ya kujitolea na sio ya kipato kikubwa kama yalivyo matarajio yenu Serikali imeelekeza kazi hii kufanyika kwa kutumia Rasilimali tulizonazo hivyo hakuna kiasi kikubwa cha fedha kilicholetwa hivyo muwe tayari kufanya kazi katika mazingira hayo” alisema Mkuu wa Wilaya
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri Bi Agnetha Mpangile aliwaasa vijana kwenda kutekeleza kazi hii kwa umakini na usahihi na kuwaambia kazi hii ilishaanza kutekezwa maeneo mengine hivyo kuna changamoto ambazo zipo katika utekelezaji kwa wanaofanya kazi hii aliwaasa kutoanzisha sheria zao wafuate maelekezo ya wataalamu watakayopewa. “tumesikia wengine wakisema wannchi wakate mahindi ili watekeleze zoezi sitarajii haya kuyasikia yamefanyika hapa Wanging’ombe vinginevyo niwatakie kazi njema “alisema Mhe Mwenyekiti wa Halmashauri
Mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku mbili tarehe 22 hadi 23/03/2022 na baada ya hapo washiriki wa mafunzo watakwenda kutekeleza kazi hiyo katika maeneo balimbali watakayopangiwa.
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.