UTAFITI WA HALI YA LISHE KWA WATOTO CHINI YA MIAKA 5 NA WANAWAKE WALIO KATIKA UMRI WA KUZAA KATI YA MIAKA 15-49
Tarehe iliyowekwa: February 9th, 2024
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wanging'ombe, Dkt. Peter Maiga Nyanja anawataarifu wananchi wote kuwa kutakuwa na zoezi la Utafiti wa Hali ya Lishe kwa Watoto wenye Umri chini ya Miaka 5 pamoja na Wanawake walio katika Umri wa Kuzaa kuanzia Miaka 15 - 49.
Hivyo Watafiti wataratibu Zoezi hili katika Ngazi ya Kaya, Vitongoji na Vijiji kuanzia Tarehe 12 hadi 24 Februari 2024, Maeneo ya Ofisi za Vijiji/Kata katika Wilaya ya Wanging'ombe.