• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za watumishi |
Wanging'ombe District Council
Wanging'ombe District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati ya Halmashauri
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha na Biashara
      • Kilimo
      • Idara ya Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Maendeleo ya Jamii
      • Idara ya Mipango na Ufuatiliaji
      • Idara ya Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu Sekondari
      • Idara ya Ujenzi
      • Idara ya Afya
      • Idara ya Maji
      • Idara ya Mazingira
      • Idara ya Ardhi na Maliasili
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Kitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Mawasiliano Serikalini
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Huduma
    • Huduma ya Maji
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha uongozi na Mipango
      • Kamati ya UKIMWI
      • Maadili
      • Uchumi,Afya na Elimu
    • Orodha ya Madiwani
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kumwona Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Miongozo
    • Fomu za Maombi
    • Gazeti la Serikali
    • Sheria ndogo za Halmashauri
    • Mpango mkakati wa Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Matukio
    • Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba

Tanzania, Rwanda Zang’ara Vita ya Rushwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) .

Tarehe iliyowekwa: February 23rd, 2018

Misimamo thabiti ya Rais John Pombe Magufuli katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya Taifa imezidi kuleta mafanikio ambapo ripoti mpya katika mapambano dhidi ya rushwa imeonesha Rwanda na Tanzania kuongoza katika ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika mapambano dhidi ya rushwa kwa mwaka 2017.
Kwa mujibu wa Ripoti ya Tathmini ya Hali ya Rushwa (Corruption Perception Index) iliyotolewa  Februari 21, 2018 na Taasisi ya Transparency International, juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano Tanzania chini ya Dkt. John Pombe Magufuli katika kupambana na rushwa zimezidi kuzaa matunda katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Taarifa hiyo iliyokusanya takwimu za mwaka mzima wa 2017 zinaonesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi chache zilizopanda kwa kiasi kikubwa katika kupambana na rushwa huku nyingi  zikishuka au kubaki pale pale.
Wakati mwaka 2016 Tanzania ilikuwa ya 116 duniani, katika ripoti hiyo mpya Tanzania imepanda kwa nafasi 13 na kuwa ya 103 huku ikizizidi kwa mbali nchi kadhaa kubwa duniani katika utafiti huo uliohusisha mataifa 180.
Aidha, kwa eneo la Afrika Mashariki, Tanzania imekuwa nchini ya pili baada ya Rwanda iliyoongoza kwa kupunguza rushwa ambapo katika alama za mtazamo wa rushwa Tanzania imepata 36, alama ambazo ni nyingi kuwahi kufikiwa na nchi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita.
Takwimu hizo zinaonesha kuwa Tanzania, kufikia nafasi hiyo ya juu, imeonesha kufanikiwa katika kufanyiakazi mianya mingi ya rushwa, kwa mujibu wa vigezo vya rushwa kupungua katika taasisi mbalimbali za Serikali na kwa mujibu pia wa mtazamo wa wafanyabiashara na wawekezaji.    
Ripoti hii inakuja ikiwa ni hivi karibuni tu Tanzania chini ya juhudi kubwa za Serikali ya Awamu ya Tano ilitajwa na ripoti ya jarida la The Economist kuongoza katika EAC kwa utawala bora na demokrasia (Democracy Index).
Akizungumzia ripoti hii jijini Dar es Salaam jana, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, alisema ripoti hiyo ni sehemu tu ya kuonesha kuwa vita dhidi ya rushwa na ufisadi nchini inafanikiwa.
“Unaweza kuyapima mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa namna nyingi katika kupambana na rushwa, ripoti hii kuonesha tumepanda kwa kuzipita nchi 13 katika mwaka mmoja ni moja tu ya ishara kuwa vita yetu hii ya haki ni ya haki kweli na inapaswa kuendelea,” alisema.
Dkt. Abbasi aliongeza,“Kama nchi tutaendelea kutekeleza. Tutaendelea kuhakikisha kile kidogo wanachokichangia wananchi kinatumika kwa maendeleo ya Taifa kama mnavyoona namna tunavyotekeleza miradi mikubwa na ya kihistoria karibu katika kila sekta.”
Hivi karibuni Ripoti nyingine ya Taasisi ya Kiuchumi Duniani (World Economic Forum) iliitaja Tanzania kuwa ya pili Afrika na ya kwanza katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara katika nyanja za uchumi jumuishi.
Mafanikio yote haya yanakuja wakati ambapo Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais aliyeahidi na anayetekeleza mageuzi, Dkt. John Pombe Magufuli, ikiwa inaendelea kwa kasi kusimamia maendeleo ya Taifa.

Matangazo

  • TANGAZO LA UMILIKISHWAJI ARDHI February 13, 2021
  • Badili Tahasusi kwa Wanafunzi Kidato cha Tano Tarajali na Vyuo vya Kati April 01, 2021
  • SIS MOBILE APPLICATION April 01, 2021
  • TANGAZO LA AJIRA LEO 09 MEI,2021 May 09, 2021
  • Itizame yote

Habari mpya

  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA VITUO VYA AFYA VITATU (3) - 1,869,307,194 /=

    May 27, 2025
  • UJIO WA MADAKTARI BINGWA WA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, HOSPITALI YA WILAYA YA WANGING'OMBE

    May 20, 2025
  • TUZO ZATOLEWA KWA WAKIMBIZA MWENGE WA UHURU 2025, NGAZI YA WILAYA - WANGING'OMBE.

    May 16, 2025
  • VIJIJI 10 VYA WANGING'OMBE KUNUFAIKA NA HATI ZA KIMILA 3,010

    May 13, 2025
  • Itizame yote

Video

MAKALA YA MIAKA MIWILI YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN WILAYA YA WANGING'OMBE
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • Vivutio vya Utalii Wanging'ombe
  • Historia ya Halmashauri ya Wanging'ombe
  • Mfumo wa Mawasiliano ya ndani wa Serikali Government Mailing System (GMS)
  • Registration Of Allied Health Professionals
  • Mfumo wa maombi ya Ajira
  • baraza la taifa la elimu ya ufundi

Tovuti Mashuhuri

  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi kwa watumishi wanaopewa ruhusa na Katibu Mkuu Kiongozi
  • Mfumo wa Malalamiko na Pongezi
  • UTUMISHI
  • MFUMO WA SIS(SCHOOL INFORMATION SYSTEM)
  • TAMISEMI
  • BUNGE

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani

Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.