Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe, Dkt. Peter Maiga Nyanja anautaarifu umma ya kuwa siku ya Jumatano 31 Januari 2024 kutakuwa na Mkutano wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kujadili taarifa ya Utekelezaji kwa Robo ya Pili kuanzia mwezi Oktoba hadi Disemba 2023.
Mkutano wa Baraza la Madiwani utatanguliwa na Baraza la Kata siku ya Jumanne tarehe 30 Januari 2024 kwa ajili ya kujadili taarifa za maendeleo ya Kata.
MAHALI/ENEO: Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe, Igwachanya.