OPERESHENI UGONJWA WA MACHO IMEFANYIKA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA - WANGING’OMBE
Tarehe iliyowekwa: November 23rd, 2023
Na. Mwandishi Wetu,
Rukia Omary,
Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika, kutoka Shirika Lisilo La Kiserikali Helen Keller, Bw. Volkan Cakir amewezesha program maalumu ya operesheni ya mtoto jicho katika Hospitali ya Wilaya ya Wanging’ombe iliyopo Kijiji cha Ihanja, Tarafa ya Mdandu.
Meneja Mradi wa Helen Keller International Bw. Athman Tawakal amesema Wizara ya Afya kushirikiana na Taasisi hii imeona Wilaya ya Wanging’ombe inauhitaji mkubwa sana wa wananchi kupatiwa huduma hii kwasababu ugonjwa huu umepelekea ulemavu wa kutoona hivyo wagonjwa watapata matibabu haya bila gharama yoyote na kuhakikisha tatizo hili linatibika kabisa na upasuaji huu unalenga kutoa matibabu kwa wagonjwa zaidi ya 500 kwa muda wa siku tano ndiyo malengo chanya ya shirika hili.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho Barnabas Mshangila ameongoza Jopo la madaktari wa magonjwa ya macho kutoka hospitali ya Rufaa Mbeya na Njombe kufanya upasuaji wa awali kuondoa mtoto jicho (ugonjwa wa macho) katika Hospitali ya Wilaya. Daktari bingwa wa Rufaa Mbeya Barnabas Mshangila amesema upasuaji huu awali ulilenga katika upasuaji wa ugonjwa wa vikope lakini ukaibuka ugonjwa mwingine wa mtoto jicho hivyo shirika hili la Helen Keller lnternational limelenga kusaidia jamii katika kutatua tatizo la ugonjwa huu wa macho ambao unaathiri kwa kiasi kikubwa mpaka kupelekea kutoona.
Mratibu wa Huduma za Macho Mkoa wa Njombe Daktari Simon Luvanda ametoa wito kwa Jamii iweke utaratibu wa kufanya vipimo vya macho marakwamara kwani ugonjwa huu wa mtoto jicho hauna maumivu yoyote isipokuwa unaathiri jicho na kupoteza nuru ya kuona kabisa kama usipochukuliwa hatua mapema.
Wananchi wa Wilaya ya Wangingombe kutoka katika kata, Vijiji na Wilaya mbalimbali Mkoani Njombe wameshukuru serikali ya awamu ya sita Ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Kushirikiana na Taasisi hii kuleta huduma vijijini na Kutatua changamoto ya ugonjwa huu wananchi wanaomba aendelee kuwajali zaidi.