Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Ally Kasinge amewaagiza viongozi katika ngazi mbambali Wilayani humo kuanzia Halmashauri hadi kwenye vitongoji kuhakikisha wanatokomeza Mimba kwa Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, Mkuu wa Wilaya ametoa agizo hilo Tarehe 14/04/2018 katika kijiji cha Igelehedza kilichopo kata ya ilembula wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazoezi kufuatia agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan.
“Naagiza kila kiongozi awajibike kwa nafasi yake kwa kubaini wanafunzi wote walio na mimba kwa kutoa taarifa na kushughulikia swala hili ili kwapamoja tutokomeze Mimba hizi lengo watoto wetu wafikie ndoto zao” alisema Mhe Mkuu wa Wilaya.
Aidha katika kutekeleza agizo hilo la kufanya mazoezi Mkuu wa Wilaya akiwa na kamati ya Ulinzi, Wakuu wa Idara,watumishi wa Halmashauri na Wananchi kwa ujumla wao waliweza kufanya mazoezi kwa kukimbia umbali wa Kilomita 14 kuanzia viwanja vya shule ya msingi Igelehedza mpaka Halali.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe aliwaasa Wananchi kuwa mazoezi hujenga afya hivyo ni vema kujiwekea utaratibu wa kufanya Mazoezi ili kuimarisha afya zetu “Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya nashauri tuweke utaratibu wa kufanya mazoezi haya mara kwa mara hata wakati Fulani kutafuta chumba maalum kwa ajili ya mazoezi” alisema Mkurugenzi.
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.