MAHAKAMA WILAYA YA WANGING'OMBE YAADHIMISHA WIKI YA SHERIA
Tarehe iliyowekwa: February 1st, 2024
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Mhe. Claudia Kitta ameshiriki Kuadhimisha siku ya Wiki ya Sheria Kitaifa ambayo imefanyika katika Mahakama ya Wilaya ya Wanging'ombe. Siku hii maalumu ya Sheria ilianzishwa na Mahakama kuu ya Tanzania kwa lengo la kutoa Elimu ya sheria kwa Wananchi ambayo hufanyika Februari, Mosi kila Mwaka.
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Mhe.Claudia Kitta amesema katika Maadhimisho hayo ya Wiki ya Sheria yaliyobeba Kauli Mbiu ya "Umuhimu wa Dhana ya Haki kwa Ustawi wa Taifa: Nafasi ya Mahakama na Wadau katika Kuboresha Mfumo Jumuishi wa Haki Jinai" MKuu wa Wilaya amefafanua ,kauli Mbiu hii inagusa maeneo yote muhimu ikiwemo kuwashirikisha wadau katika mpango wa utoaji Haki.
Akatilia mkazo Kwa kuwaagiza wanasheria na Viongozi mbalimbali katika Wilaya watumie Elimu hii ya sheria katika kutatua makosa ya Jinai yanayofanyika katika jamii zetu na kuyafumbia macho hasa ukatili wa kijinsia, mauaji, masuala ya rushwa,ubakaji na Imani potofu.Jamii zetu zimekuwa na uoga wa kuripoti matukio ya kikatili yanayofanyika kwa kuhofia kutoa ushahidi pale sheria inapochukua hatua zaidi dhidi ya ripoti hizo hivyo wananchi wawe huru kutoa taarifa na sheria zitakulinda .
Aidha, Mwanasheria MKuu wa Mahakama ya Wilaya Bw.James Emmanuel Mhoni amefafanua kuwa wiki ya Sheria ni kiashiria Cha kuanza kwa shughuli za sheria hivyo sheria inatoa fursa kwa Wananchi kujifunza umuhimu wa sheria na kutambua majukumu ya Mahakama jinsi inavyotumia sheria hizo kutekeleza majukumu ya kazi zake na zinavyomsaidia mwananchi katika kutafuta Haki na kupata Elimu kuhusu sheria hii itawafungulia njia ya kujiamini na kufika mahakamani kuwasilisha kesi zenu zote zitasikilizwa.
Maadhimisho hayo ya Wiki ya sheria yamehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Kisiasa, Katibu Tawala Wilaya,Mkurugenzi Mtendaji , Jeshi la Wananchi, Jeshi la kujenga Taifa, Jeshi la Akiba, Viongozi wa Dini mbalimbali Wanafunzi na Wananchi wa kutoka vijiji na Kata mbalimbali Kuungana Kuadhimisha.