KIKAO CHA MPANGO WA AWALI BAJETI YA LISHE 2024 - 2025
Tarehe iliyowekwa: November 28th, 2023
Na. Mwandishi Wetu,
Rukia Omary,
Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe kupitia Idara Ya Afya imefanya kikao kazi cha kuandaa mpango bajeti wa utekelezaji wa awali wa huduma za lishe mtambuka mwaka wa fedha 2024/2025
Akizungumza katika kikao hicho Mganga Mkuu wa Wilaya Bw. Frank Chiduo amesema ni muhimu katika uandaaji wa mpango kazi kuzingatia vipaumbele ambavyo vitasaidia kuboresha masuala ya lishe hasa katika utoaji elimu ya lishe mtambuka kwa wananchi. Akatilia mkazo masuala ya lishe kipindi cha nyuma ambayo hayakufanyika kwa sasa ndio yapewe kipaumbele na marekebisho yote ambayo yamefanyika katika kuweka maboresho ya mpango kazi ujao yakazingatiwa ili kupata mpango kazi utakaoleta tija kwa wananchi.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Lishe kwa mwaka 2022-2023 na robo ya kwanza ya 2023/2024 Afisa Lishe Wilaya Bi Zenobia Aloyce ili kuhakikisha lishe inakuwa ni mtambuka kitengo cha lishe kimefanikiwa kuwafikia wananchi kwa kutoa elimu ya lishe na kuwashirikisha viongozi wa serikali katika siku ya afya na lishe katika ngazi ya mitaa na Kata.
Kwa upande wake afisa lishe Mkoa Bi. Bertha Nyigu amesema suala la lishe litaambatana na mafunzo ya matibabu ya utapiamlo kwa watoa huduma za afya pia utoaji wa elimu ya afya na lishe mashuleni,na kwenye jamii kwa kuanzisha club za lishe katika shule mbalimbali. Pia wadau mbalimbali tunaomba wajitokeze kushirikiana na Idara ya Afya ili kuwezesha mpango huu lishe kutekelezeka.
Aidha, idara za afya katika mpango wa awali wa huduma za lishe idara na vitengo vingine vya kilimo na mifugo,uvuvi,elimu msingi na sekondari maendeleo ya jamii na ustawi wa jamii, mipango na uchumi kushirikiana ili kutekeleza azimio la mpango bajeti wa lishe na utekelezaji.