KAMPENI YA UZINDUZI WA LISHE YAFANYIKA WILAYA YA WANGING'OMBE
Tarehe iliyowekwa: January 25th, 2024
Na. Mwandishi Wetu,
Rukia Omary
Katika kuhakikisha udumavu ndani ya Wilaya ya Wanging'ombe unatokomezwa wananchi katika Wilaya ya Wanging’ombe wamejitokeza kwa wingi kuweza kusikiliza na kupata Elimu juu ya lishe,Wananchi hao wamejitokeza katika viwanja vya Soko Makao makuu ya Halmashauri ambapo mkutano huo umeandaliwa na viongozi katika Wilaya ya Wanging'ombe.
Mkutano huo umehudhuriwa na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Wanging’ombe Mhe. Mkuu wa Mkoa amewaasa wananchi kuhakikisha wanapata chakula chenye makundi yote na kuacha tabia ya Kuwapa pombe watoto pindi wanapokuwa kwenye shughuli zao kwani kwa kufanya hivyo watoto wanakosa virutubisho mwilini na kuwa wadumavu, amewaomba wananchi kila moja kwa nafasi yake kuhakikisha wanapambana na tatizo hilo la udumavu ili kuwezesha kuwa na kizazi chenye afya siku zijazo.
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali ndani ya Wilaya ambapo Bi Veronica Gerald Sanga ambae ni katibu Tawala wa Wilaya ya Wanging'ombe akimwakilisha Mhe. Mkuu wa Wilaya amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa wananchi wa Wanging'ombe wanamapokeo chanya juu ya jitihada za kutokomeza udumavu ambapo kwa sasa imekuwa ni agenda ya kudumu katika vikao namikutano mbalimbali, Katibu Tawala amewashukuru wadau mbalimbali ambao wamejitokeza kuunga mkono kampeni za kutokomeza Udumavu.
Katibu Tawala amesema kauli mbiu yetu ya kujaza tumbo sio lishe Jali unachokula inatoa hamasa kubwa ya kupambambana na Udumavu kwa sababu Mkoa wa Njombe umebarikiwa kuwa na vyakula vya kutosha na vya kila aina hivyo ni wajibu wetu wananchi wa Wanging'ombe kula kwa kufuata kanuni za lishe ili kuhakikisha vyakula tulivyonavyo vinaboresha afya zetu.
Aidha , viongozi wa dini wameipongeza Serikali ya Wilaya ya Wanging’ombe pamoja na Mkoa kwa kufanya mikutano hiyo ya kuhamasisha wananchi kupambana na udumavu wamewaomba wananchi wenzao kuzingatia elimu hiyo na kuhakikisha kila moja katika familia yake anaweka utaratibu wa kupata lishe bora ili kuwezesha familia kuwa na Afya njema na kisha kutokomeza Udumavu.