Na. Baraka Tarimo,
MKUU wa wilaya ya Wanging'ombe, Mhe. Zakaria Mwansasu ametoa elimu ya utekelezaji wa bima ya afya kwa wote (NHIF) ikiwa lengo ni kuwajengea uwezo wadau wa afya ili kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo.
Elimu hiyo imetolewa leo tarehe 06 Februari 2026 katika Ukumbi wa Halmashauri, ambapo Mhe. Mwansasu amesema katika siku 100 za uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi bima ya afya kwa wote (NHIF) kwa lengo kuhakikisha usalama wa afya kwa wananchi wake.
Imeelezwa ya kuwa “Faida za kujiunga na mfuko wa bima ya afya kwa wote (NHIF) ni pamoja gharama nafuu ambapo kifurushi cha shilingi 150,000/= kinahudumia watu sita (Baba, Mama na Watoto/Ndugu/Wazazi wanne) kwa mwaka mmoja. Pia katika kifurushi hicho utapata huduma za vipimo 43 vya maabara, vipimo 37 vya radiolojia, huduma za dawa na vifaa tiba 247, huduma za upasuaji mkubwa na mdogo 37 pamoja na huduma za rufaa kuanzia ngazi Zahanati hadi Hospitali ya taifa”.
Aidha wadau wa Afya baada ya kupokea elimu hiyo wameshauri ya kuwa uboreshaji wa mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ni muhimu ili kuendana na kasi ya utoaji huduma bora ila pia kupunguza urasimu wakati wa utoaji wa huduma za afya.










Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.