KATIBU Tawala, Mkoa wa Njombe, Dkt. Stephen Nindi ameahidi kufanya mkoa wa Njombe kuendelea kuwa wa kipekee zaidi kwa kujikita zaidi kwenye ubunifu na juhudi katika kazi ili kufika ndoto za wana Njombe.
Akizungumza hayo wakati wa hafla fupi ya mapokezi yake, Dkt. Nindi amesema atatumia uzoefu alioupata katika taasisi mbalimbali za Serikali kuhakikisha Mkoa wa Njombe unakua kiuchumi, hususani kupitia fursa zilizopo katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi, sekta ya madini, maliasili, uwepo wa hali ya hewa nzuri na uchapakazi wa wana Njombe.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Antony Mtaka, amewataka viongozi wote mkoani Njombe kuhakikisha wanakuwa wabunifu katika utekelezaji wa majukumu yao, kwa kuwa wananchi wanahitaji matokeo.




Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.