CMT WANGING’OMBE YATEMBELEA MIRADI YENYE THAMANI YA BILIONI 2.8.
Tarehe iliyowekwa: October 16th, 2025
Na. Nickson Kombe,
KAMATI ya Watalamu (CMT) ya Halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe yatembelea Miradi ya sekta ya Afya na Elimu yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.8 katika kata za Igosi, Imalinyi, Luduga, Ilembula na Uhambule.
Akitolea ufafanuzi wa ziara hiyo tarehe 15 Oktoba 2025, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Wakili Joshua Sanga amesema zoezi la ukaguzi wa miradi hiyo ni kuendelea kufanya ufuatiliaji wa karibu ili kuhakikisha miradi inakamilishwa kwa wakati na ubora unaostahili ambapo wananchi kupatiwa huduma bora za afya na elimu mapema iwezekanavyo.
Katika ziara hiyo Wakuu wa Idara na Vitengo walitembelea kata ya 5 ambazo ni Kituo cha Afya – Igosi – Milioni 623 (Igosi), Shule ya Msingi Imalinyi Mkondo B – Milioni 323 (Imalinyi), Kituo cha Afya Luduga – Milioni 623 (Luduga), Shule ya msingi Igheledza Mkondo B – Milioni 323 (Ilembula) na Kituo cha Afya Uhambule – Milioni 623 (Uhambule). Ambapo miradi yote mitano ina thamani ya Bilioni 2.8.
Aidha ziara ya Ukaguzi wa miradi ni endelevu ikiwa lengo ni kuwawezesha menejimenti ya Halmashauri kuendelea kufuatilia na kusimamia ipasavyo ili kupata miradi iliyobora zaidi kwa kuzingatia muda wa utekelezaji miradi hiyo ambapo wananchi wa wilaya ya Wanging’ombe watanufaika zaidi na huduma mbalimbali katika miradi hiyo.