PL.3 JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA AHADI YA UADILIFU KWA VIONGOZI WA UMMA Kwa kuzingatia misingi ya maadili iliyoainishwa katika Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995, ambayo yanamtaka kila kiongozi wa umma kuzingatia viwango vya juu vya maadili ili kukuza utu, uwazi, uadilifu, uwajibikaji na kuimarisha imani ya wananchi kuhusu utendaji wa Serikali; Mimi.............................................................................. ninaahidi umma kwamba: 1. Nitakuwa mzalendo kwa nchi yangu na mtii kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; 2. Nitakuwa muadilifu na mfano kwa watumishi wa umma na watu wengine katika kukuza na kusimamia maadili; 3. Sitatumia cheo changu au wadhifa wangu kwa masilahi binafsi, ya familia yangu, ndugu zangu au marafiki zangu isipokuwa kwa maslahi ya umma; 4. Nitalinda na kutumia rasilimali za umma kwa maslahi ya umma; 5. Nitatekeleza majukumu yangu na kufanya maamuzi kwa kuzingatia Sera, Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo kwa maslahi ya umma; 6. Sitaomba, kushawishi, kutoa wala kupokea rushwa; 7. Sitaomba, kutoa wala kupokea zawadi au fadhila za kiuchumi au za kisiasa au kijamii zisizoruhusiwa na Sheria; 8. Sitatoa shinikizo kinyume na Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo katika utendaji kazi za umma, hususan ajira, kupandisha cheo, kuchukua hatua za kinidhamu au kuingia mikataba mbalimbali; 9. Sitatoa taarifa za siri za Serikali au za mteja kwa watu wasiohusika isipokuwa kwa maslahi ya umma; 10. Nitatekeleza majukumu yangu kwa kuepusha mgongano wa maslahi wa aina yoyote na endapo utatokea uamuzi wangu utazingatia masilahi ya umma; 11. Nitatoa huduma bora kwa usawa kwa watu wote bila kujali misingi ya dini, siasa, kabila, udugu, ukanda, jinsia, urafiki au hali ya mtu; 12. Nitaepuka tabia ambayo inavunja heshima ya uongozi wa umma hata ninapokuwa nje ya mahali pa kazi au nitakapoacha kazi. Tamko: Ninakiri kwamba nimeisoma Hati hii ya Ahadi ya Uadilifu kabla ya kuweka sahihi. Ninakubaliana na kutambua kwamba masharti yaliyo katika Hati hii ni ya kimaadili na kisheria na ninawajibika kuyatekeleza. Ninaelewa kwamba ukiukwaji wa masharti hayo ni ukiukwaji wa maadili yaliyowekwa kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, masharti ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Sheria ya Utumishi wa Umma, Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sheria ya Kudhibiti Mgongano wa Masilahi na Sheria nyingine za nchi na hatua za kisheria zinaweza kuchukuliwa dhidi yangu iwapo nitakiuka masharti hayo. ............................................. ................. ................... .................... JINA WADHIFA SAINI TAREHE .............................................. .................. .................. KAMISHNA WA MAADILI SAINI TAREHE