Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe pamoja na wataalamu wamepongezwa kwa Ujenzi unaoridhisha wa Jengo la Nanenane lililopo katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya kwa kutumia mapato ya Ndani ya Halmashauri, pongezi hizo zimetolewa na Mhe Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe Comrade Ally Kassinge leo Jijini Mbeya Wakati alipo ungana na Kamati ya Fedha kukagua Ujenzi wa Jengo la Nanenane ikiwa ni ziara ya Ukaguzi wa miradi kwa robo ya nne. “Mhe Mwenyekiti tangu nifike Wilaya ya Wanging’ombe mapato ya ndani yamekuwa yakiongezea mwaka hadi mwaka hata kupelekea umaliziaji wa jengo hili kuendelea, ni rai yangu kwenu kuhakikisha Kamati yako pamoja na Wataalamu mnatumia mapato ya ndani kutekeleza miradi ya maendeleo vijijini ili Wananchi waone faida ya mapato hayo” alisema Kasinge.
Akitoa neno la shukrani Mhe Mwenyekiti wa Halmashauri Anthon Mahwata alipongeza jitihada za Wataalamu katika kusimamia shughuli za Ujenzi huo na kusema thamani ya Fedha inaonekana, “Nawataka wataalamu kuendelea kusimamia miradi mingine inayotekelezwa katika Halmashauri yetu vizuri na kwa weredi”alisema Mhe Mahwata.Aidha Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Ndg Emmanueli Kilundo alipokea maelekezo na pongezi hizo kwa niaba ya wataaalamu wa Halmashauri na kusema yote walioshauri yatazingatiwa katika utekelezaji.Katika ziara hiyo wajumbe pia waliagiza wataalamu kuandaa Taarifa ya gharama ya Ujenzi wa jengo hilo mpaka kukamiliaka, aidha ilifaafanuliwa kuwa Ujenzi huo mara ya kwanza Halmashauri iliingia Mkataba na Mkandarasi Chelesi lakini baadae baada ya maelekezo ya Serikali kusisitiza kutumia Utaratibu wa kuchangia jitihada za Serikali Halmashauri iliamua kuvunja Mkataba na kuanza kutekeleza yenyewe kwa kutumia mafundi wa kawaida Ujenzi huu unategemewa kugharimu takribani Tsh 85,000,000/=
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.