Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe anawatangazia wananchi wote wa Wilaya ya wanging'ombe kuwa Mwenge wa Uhuru utakimbizwa Wilayani tarehe 29/05/2018, ukiwa Wilayani Mwenge wa uhuru utakagua,kuzindua na kuweka mawe ya Msingi kwenye miradi mbalimbali ndani ya Halmashauri, aidha mwenge huo utapokelewa kijiji cha Itulahumba ukitokea Halmashauri ya Mji Makambako, mwenge wa uhuru utapita katika vijiji vifuatavyo Itulahumba,wanike,mngate,imalinyi,gonelamafuta,kidugala,mtapa,chalowe,igwachanya,udonja,mpululu,wangutwa,itandula na kukesha katika kijiji cha Wanging'ombe Mkurugenzi anawaomba wananchi kujitokeza katika kuulaki Mwenge wa Uhurunkwenye maeneo yote utakakopita na kukesha.
Copyright ©2021 Wanging'ombedc . All rights reserved.